October 24, 2021

Mbunge wa jimbo la Busanda mkoani Geita, Mhe. Tumaini Magessa amesema kuna haja ya kuwa na kampeni ya nchi nzima kuhamasisha ufungamanishaji wa sekta ya madini na sekta nyingine hususani kilimo ili kuwa na uchumi endelevu. Magesa amesema hayo Oktoba 24, 2021 wakati alipotembelea banda la asasi ya.....

Bado ni Changamoto Ufungamanishaji wa Sekta ya Madini na Kilimo
Mbunge wa jimbo la Busanda mkoani Geita, Mhe. Tumaini Magessa amesema kuna haja ya kuwa na kampeni ya nchi nzima kuhamasisha ufungamanishaji wa sekta ya madini na sekta nyingine hususani kilimo ili kuwa na uchumi endelevu.

Magesa amesema hayo Oktoba 24, 2021 wakati alipotembelea banda la asasi ya HakiRasilimali wakati wa maonyesho ya Wiki ya Azaki 2021 ambayo yanaendelea jijini Dodoma.

"Katika maeneo ninayotoka shughuli za uchimbaji wa dhahabu zimekuza miji na kuimarisha biashara. Pesa inayopatikana kwenye uchimbaji imeimarisha na kuibua biashara nyingine zikiwemo za maduka", amesema Mhe. Magessa.

Ameongeza kuwa, "Licha ya biashara hizo zilizoibuka lakini eneo la kilimo bado haliridhishi, bado pesa zinazotoka kwenye madini hatujaweza kuzipeleka kwenye kuinua kilimo ambacho ndicho nguzo kuu ya uchumi. Hili ni jambo ambalo linapaswa kuwa kampeni ya nchi nzima katika maeneo yenye shughuli za uchimbaji".

Related Posts

JUKWAA LA UZIDUAJI 2026
Oct 19, 2026

JUKWAA LA UZIDUAJI 2026

HakiRasilimali is pleased to announce Jukwaa la Uziduaji 2026, taking place on 12–13 November 2026 in Dodoma, Tanzania. Under the theme “From Natural...

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi) 2026
Jul 21, 2026

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi) 2026

About the Programme ESKi Tanzania is a capacity development programme designed to nurture and empower the next generation of leaders, community advoca...

CALL FOR ABSTRACTS
Jun 12, 2026

CALL FOR ABSTRACTS

📢 CALL FOR ABSTRACTS HakiRasilimali invites researchers, academics, practitioners, policymakers, and civil society actors to submit abstracts for th...